Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Baraza la Usalama kwenye kikao chake cha awali kwa mwezi huu, limepitisha ajenda ya kazi kwa Disemba. Baada ya hapo Baraza limepitisha azimio linaloruhusu, kwa muda wa miezi 12, Mataifa na mashirika ya kikanda kuingiza vyombo vyao katika maeneo ya mipaka ya bahari ya Usomali, kwa lengo la kukomesha vitendo vya uharamia na wizi wa kutumia silaha unaofanyika kwenye mwambao wa taifa hilo. ~~

Hapa na Pale

Ijumatatu, KM Ban Ki-moon ametangaza kumteua Michel Sidibé wa Mali, kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Jumuiya ya Kusimamia Miradi ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS). Sidibé anatazamiwa kuanza kazi tarehe 1 Januari 2009.

Mkutano wa kugharamia maendeleo wakaribia hatima

Mkutano wa Kimataifa juu ya Ugharamiaji wa Maendeleo unaofanyika kwenye mji wa Doha, Qatar leo umeingia siku ya tatu na unakaribia kuhitimishwa. Kikao kinafanya mapitio ya mapendekezo yaliopitishwa 2002 kwenye mkutano wa Monterrey, Mexico; mapatano yalioafikiana kuwepo ushirikiano mkubwa baina ya nchi zenye maendeleo ya viwanda na nchi maskini kugharamia misaada ya maendeleo, hasa katika kuandaa misaada rasmi ya kigeni, masharti ya kibiashara yanayoridhisha na kusamehe madeni ya nchi zinazoendelea. KM kwenye risala yake alitilia mkazo umuhimu wa “kuhakikisha watoto wote huwa wanafadhiliwa ilimu ya msingi, ilimu ambayo ikikosekana nchi husika zinazoendelea zitashindwa kukamilisha malengo yao ya maendeleo.” Alisema watoto milioni 75 duniani, hivi sasa, wamenyiwa fursa ya kupata ilimu, na mamilioni ziada katika mataifa masikini hupatiwa ilimu, lakini ya kiwango cha chini kabisa kuwawezesha wao kujihudumia kimaisha.

UM unaihishimu Disemba mosi kuwa Siku ya UKIMWI Duniani

Tarehe ya leo, Disemba mosi, inahishimiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ni Siku ya UKIMWI Duniani; na taadhima za mwaka huu zinakamilisha miaka 20 tangu UM kuanzisha kampeni ya kuhimiza Mataifa Wanachama kuchangisha huduma zao kupambana kipamoja na janga hili kote ulimwenguni. Kwenye ripoti iliotolewa na Jumuiya ya Muungano wa Miradi ya Mashirikia ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) ilikumbusha kwamba katika kipindi kilichomalizikia 2007, watu milioni 33 walikadiriwa kuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI katika dunia.