Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za binadamu lalaani ukiukaji wa haki za kimsingi dhidi ya raia katika JKK

Baraza la Haki za binadamu lalaani ukiukaji wa haki za kimsingi dhidi ya raia katika JKK

Baraza la Haki za Binadamu, ambalo tangu wiki iliopita lilikutana mjini Geneva, Uswiss kujadilia masuala yanayohusu utekelezaji wa haki za binadamu kwenye eneo la mashariki, katika JKK, leo limetoa taarifa ilioshtumu na kulaani vikali, ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia, ulioonekana kuendelezwa kwenye sehemu hizo za nchi katika wiki za karibuni.