Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafutaji wa ajira kukidhi maisha ndio unaohamasisha umma wa kimataifa kuhama makwao, imebainisha ripoti ya IOM

Utafutaji wa ajira kukidhi maisha ndio unaohamasisha umma wa kimataifa kuhama makwao, imebainisha ripoti ya IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Uhamaji (IMO) leo limewasilisha Ripoti ya Uhamaji kwa 2008 ambayo ilibainisha uhamaji mkubwa wa karne ya 21 unasababishwa zaidi na ile sera ya kusawazisha uchumi kwenye soko la kimataifa, hali ambayo huwalazimisha watu kuhama makwao na kuvuka mipaka kutafuta rizki ya kukidhi mahitaji yao kiuchumi na jamii.