Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kugharamia maendeleo wakaribia hatima

Mkutano wa kugharamia maendeleo wakaribia hatima

Mkutano wa Kimataifa juu ya Ugharamiaji wa Maendeleo unaofanyika kwenye mji wa Doha, Qatar leo umeingia siku ya tatu na unakaribia kuhitimishwa. Kikao kinafanya mapitio ya mapendekezo yaliopitishwa 2002 kwenye mkutano wa Monterrey, Mexico; mapatano yalioafikiana kuwepo ushirikiano mkubwa baina ya nchi zenye maendeleo ya viwanda na nchi maskini kugharamia misaada ya maendeleo, hasa katika kuandaa misaada rasmi ya kigeni, masharti ya kibiashara yanayoridhisha na kusamehe madeni ya nchi zinazoendelea. KM kwenye risala yake alitilia mkazo umuhimu wa “kuhakikisha watoto wote huwa wanafadhiliwa ilimu ya msingi, ilimu ambayo ikikosekana nchi husika zinazoendelea zitashindwa kukamilisha malengo yao ya maendeleo.” Alisema watoto milioni 75 duniani, hivi sasa, wamenyiwa fursa ya kupata ilimu, na mamilioni ziada katika mataifa masikini hupatiwa ilimu, lakini ya kiwango cha chini kabisa kuwawezesha wao kujihudumia kimaisha.