Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ngirabatware amekana makosa ya jinai ya halaiki Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imeripoti ya kwamba Augustin Ngirabatware, aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Nchi Rwanda Ijumaa alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kukabili mashitaka alikana makosa kumi ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki nchini mwao katika miaka ya 1990, jinai ambayo inasemekana ilikiuka sheria ya kiutu ya kimataifa.

Hapa na Pale

Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) imeripoti hali ya chakula Ethiopia inaendelea kuharibika. Kwa mujibu wamakadirio ya laribuni ya Serikali ya Ethiopia na washiriki wenzi wa huduma za kiutu watu milioni 6.4 wanahitajia kufadhiliwa misaada ya dharura ya chakula kwa sasa angalau kunusuru maisha. Huo ni muongezeko wa asilimia 40 tangu Juni 2008. Kwa sababu hiyo, watu wingi zaidi wanahamia mijini kutafuta chakula kutokea vijijini. Vitovu vitatu vya ugawaji chakula kwa umma muhitaji vinatayarishwa kwa sasa kuwapatia posho inayofaa karibu watu milioni mbili muhitaji wanaoishi kwenye eneo husika. Mashirika ya UM ya WHO na UNICEF nayo pia yamejumuisha mchango wao kudhibiti miripuko ya magonjwa ya kuambukiza.

UNHCR imefichua mapengo kwenye huduma za kimsingi kwa wahamiaji duniani

L. Craig Johnstone, Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Alkhamisi aliwasilisha ripoti yenye kuonyesha kuwepo pengo kubwa katika utekelezaji wa ule mradi wa majaribio ya kukidhia mahitaji halisi ya wahamiaji katika mataifa manane yanayohudumiwa na UNHCR – ikijumlisha Cameroon, Ecuador, Georgia, Rwanda, Thailand, Tanzania, Yemen and Zambia.

Hapa na Pale

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeripoti Alkhamisi kuwa Jamhuri ya Kideokrasi ya Umma wa Korea (DPRK), ambayo pia hujulikana kama Korea ya Kaskazini, imearifu rasmi kwamba wataalamu wa IAEA hawaruhusiwi tena kukagua viwanda vya kinyuklia viliopo Yongbyon kuanzia hivi sasa. Kadhalika DPRK imearifu kwamba imesitisha zile shughuli za kulemaza huduma za kinyuklia katika Yongbyon, shughuli ambazo zitafufuliwa tena karibuni, kinyume na yale makubaliano yaliofikiwa baada ya Mazungumzo ya Pande Sita. Shirika la IAEA limesema litasalia Yongbyon kusibiri taarifa ziada kutoka Serikali ya DPRK.

Wakulima wa kiasilia warahisishiwa biashara na UM

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza vyombo viwili vipya vya kuwasaidia wakulima wanaotumia mbolea za kimaumbile kuuza bidhaa zao kwenye soko la kimataifa bila ya pingamizi. Vifaa hivi ni matunda ya ushirikiano wa utafiti wa miaka sita miongoni mwa wataalamu wa FAO, Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) na pia Shirikisho la Kimataifa la Wakulima Wanaotumia Mbolea za Kimaumbile (IFOAM) na vinatarajiwa kuwasilisha mapokezi bora ya mazao yaliyooteshwa kimaumbile katika soko la kimataifa.

Waziri wa zamani Rwanda ahamishiwa kizuizini Arusha

Waziri wa zamani wa Miradi ya Nchi Rwanda, Augustin Ngirabatware, anayekabili mashitaka ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki na ukiukaji mbaya wa kanuni za kiutu za kimataifa, Ijumatano amehamishwa kutoka Frankfurt, Ujerumani, alipokamatwa wiki mbili zilizopita, na kupelekwa kwenye Kituo cha Kufungia Watu cha Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kilichopo Arusha, katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.