Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Uchumi wa 2008 duniani ni wa gizagiza, inasema UNCTAD

Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) limetoa ripoti ya mwaka inayozingatia \'hali ya biashara na maendeleo kimataifa kwa 2008\'. Ripoti ilisema katika miaka ya karibuni nchi nyingi zinazoendelea zilionekana kufanikiwa kwenye maendeleo yao ya uchumi yenye kutia moyo.

Mkutano wa DPI/NGO Paris unazingatia biashara haramu ya watoto

Mkutano wa Idara ya Habari ya UM na mashirika yasio ya kiserikali unaofanyika Paris, Ufaransa katika siku ya pili ya majadiliano, Alkhamisi mashauriano yalilenga zaidi kwenye tatizo la biashara karaha ya watoto wadogo ambao hutekwa nyara na majambazi,na baadye huvushwa mipaka kutopka makwao na hutumiwa kwenye vitendo haramu vyenye kuwanyima watoto hao haki za kimsingi na utu wao. Mathalan, watoto hawa wenye umri mdogo hulazimishwa kufanya kazi zisiolingana na umri wao, na mar nyengine hushirikishwa kwenye vitendo karaha vya kuwafanya watoto hawa kuwa watumwa wa uzinzi. ~

HAPA NA PALE

UM umetangaza kuwa sasa hivi unaweza kuthibitisha kihakika kwamba maiti 17 zimeonekana karibu na eneo lilipotukia ajali ya ndege iliokodiwa na UM , nje ya mji wa Bukavu, katika mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo JKK). UM unajitayarisha, kwa sasa, kuendeleza shughuli za kuchunguza utambulisho wa mabaki ya maiti. Miongoni mwa waathiriwa hao walikuwemo raia wanne wa Kongo pamoja na raia mmoja wa Kanada, watumishi wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP).

Usomali inahimizwa kurudisha amani wakati wa Ramadhan

Mark Bowden, Mshauri Mkaazi wa UM juu ya Misaada ya Dharura kwa Usomali ametuma salamu maalumu, kwa niaba ya jamii ya UM, kutokea ofisi yao iliopo Nairobi, Kenya zilioukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia umma wa Usomali Ukarimu Mkuu kwa Ramadhan ya mwaka huu.

'Mpaka wa mwisho' wa uvuvi wahitajia usimamizi bora, FAO kuonya

Baada ya miaka miwili ya mashaurianio na majadiliano, wiki hii wajumbe wanachama wa mataifa 191 wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wamefanikiwa kuafikiana na kupitisha miongozo mipya ya kimataifa ili kudhibiti bora uvuvi, hasa ule uvuvi wa kina kikubwa baharini, ambapo mfumo wa ikolojia ni dhaifu na haraka kuharibika kama haujatunzwa kama inavyotakikana kisayansi.