Skip to main content

Faraja ya madeni haitoshelezi pekee kufyeka hali duni ulimwenguni, inahadharisha Tume ya MDGs

Faraja ya madeni haitoshelezi pekee kufyeka hali duni ulimwenguni, inahadharisha Tume ya MDGs

Tume Maalumu ya Kusimamia Utekelezaji wa Dharura wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), iliobuniwa na KM Ban Ki-moon, imewasilisha ripoti maalumu yenye kuelezea matokeo ya utafiti juu ya utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na jumuiya ya kimataifa za kuzisaidia nchi maskini kupunguza hali duni kwa nusu itakapofika 2015.

Ripoti ilisema wahisani wa kimataifa watahitajia kuongeza misaada ya maendeleo kwa kima cha dola bilioni 18 kila mwaka, kuanzia hivi sasa hadi 2010, ili kuziwezesha nchi maskini kukamilisha Malengo ya MDGs kama ilivyodhamiriwa. Baadaye mwezi huu viongozi wa dunia watakusanyika kwenye Makao Makuu, mjini New York, ya UM kufanya mapitio juu ya maendeleo kuhusu utekelezaji wa Malengo ya MDGs. Ripoti iliwasilishwa rasmi na KM wakati nilipokuwa ninaelekea studio. Tutakupatieni maelezo zaidi kwenye taarifa zetu za wiki.