Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu linazingatia pendekezo la kupiga vita ugaidi duniani

Baraza Kuu linazingatia pendekezo la kupiga vita ugaidi duniani

Baraza Kuu la UM limekutana wiki hii kwa siku mbili, kwenye kikao cha wawakilishi wote kuzingatia azimio la kupiga vita ugaidi duniani. Kulifanyika majadiliano maalumu yaliofanya mapitio juu ya lile azimio la 2006 la Kuratibu Mipango ya Pamoja Kupiga Vita Ugaidi Ulimwenguni.

Wajumbe walioshiriki kwenye mjadala wa Baraza Kuu walibainisha aina ya uzoefu wanaotumia kitaifa kukabiliana na matatizo sugu ya kigaidi.

KM Ban Ki-moon, kwenye risala yake alioitoa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu, aliyataka Mataifa Wanachama kuchukua mtazamo tofauti pale yanapokabiliana na suala la ugaidi, yaani mwelekeo utakaokuwa "na ukweli imara, na utakaotegemewa kuwa na fusa ya utendaji” itakayoshirikisha wahusika wengi wa kimataifa.

Sikiliza maelezo kamili kwenye idhaa ya mtandao.