Ripoti 2008 ya UNAIDS juu ya UKIMWI duniani ni ya mchanganyiko
Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) imewakilisha rasmi hapa Makao Makuu ripoti ya 2008 iliofanya mapitio juu ya maendeleo katika kupiga vita maradhi ya UKIMWI ulimwenguni. Ripoti imesema UNAIDS imekadiria katika 2007 watu milioni 33 ulimwenguni walikuwa wakiishi na virusi vya UKIMWI; na wakati huo huo watu milioni 2.7 waliambukizwa na VVU, na milioni 2 ziada walifariki kwa sababu kadha wa kadha zinazoambatana na UKIMWI.