Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inasema kunyonyesha watoto kunafaidisha afya

UNICEF inasema kunyonyesha watoto kunafaidisha afya

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Umoja wa WABA ambao huendeleza miradi ya kimataifa ya unyonyeshaji, wametoa mwito wa pamoja unaopendekeza kuongezwe misaada ya miradi ya kuwahimiza akina mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto wao ili kuwakinga watoto wachanga na maambukizo ya magonjwa hatari na maututi ya kitoto.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashirika hayo mama wanaoamua kunyonyesha watoto wachanga katika miezi sita ya kwanza baada ya watoto kuzaliwa, husaidia kuwapatia watoto hawo kinga imara na hifadhi bora dhidi ya matatizo yanayoletwa na utapiamlo na huwakinga na maradhi maututi ya utotoni.