Skip to main content

UM kukomesha ulinzi wa amani mipakani ETHIOPIA/ERITREA

UM kukomesha ulinzi wa amani mipakani ETHIOPIA/ERITREA

Baraza la Usalama lilikutana mapema asubuhi kuzingatia azimio nambari 1827 (2008) liliopendekezwa na Ubelgiji, la kukomesha shughuli za kulinda amani na uangalizi wa kusitisha mapigano za Shirika la UNMEE mipakani baina ya Ethiopia na Eritrea. Azimio limepitishwa, bila kupingwa na wajumbe wote 15, na limependekeza kusisitisha shughuli za UNMEE kieneo kuanzia Alkhamisi, tarehe 31 Julai 2008.

Baraza la Usalama limeamrisha Ethiopia na Eritrea kukamilisha kutekeleza majukumu yao chini ya Maafikiano ya Algiers, na kutakiwa waonyeshe ustahamilivu wa hali ya juu kwa kujizuia na vitisho na kutumia nguvu baina yao, na pia kunasihiwa kujiepusha na uchokozi wa vitendo vya kijeshi. Azimio limetaka KM ashauriane na Ethiopia na Eritrea juu ya uwezekano wa UM kuwepo kwenye maeneo yao kuimarisha usalama na amani.