Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ghana kuongoza Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba

Ghana imekabidhiwa uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba. Mwakilishi wa Kudumu wa Ghana katika UM, Balozi Leslie Kojo Christian aliitisha mkutano wa waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ambapo aliwaarifu kuhusu ajenda ya vikao vijavyo kwa mwezi Oktoba. Balozi Christian alidhihirisha ya kuwa ajenda ya mijadala italenga zaidi yale matatizo yanayohusu hali katika Usomali na Cote d’Ivoire, na pia alitarajia kusailiwa masuala juu ya haki za wanawake, pamoja na mada zinazoambatana na juhudi za kimataifa za kuimarisha usalama na amani duniani.

UM bado kuendeleza operesheni za kihali kwa waathiriwa wa mafuriko Uganda

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura Duniani (OCHA) imeripoti mafuriko bado yanaendelea kuisumbua Uganda, hali ambayo imeilazimisha UM kuendeleza zile operesheni za kuhudumia misaada ya kihali ya kunusuru maisha ya raia waathiriwa na janga hili la kimaumbile. OCHA imeripoti kuhitajia mchango ziada wa dharura, kuweza kukidhia mahitaji ya kimaisha ya umma husika.

Huduma za kiutu zimeanzishwa tena na UM Kivu Kaskazini

Watumishi wa UM wanaohudumia misaada ya kiutu Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wiki hii walifanikiwa kuwafikia wale wahamiaji wa ndani ya nchi walionyimwa mahitaji yao ya kihali katika siku za nyuma, kwa sababu ya kufumka kwenye maeneo yao mapigano kati ya vikosi vya Serekali na waasi.

Liberia inastahili msaada wa Mfuko wa Ujenzi wa Amani: asema KM

KM Ban Ki-moon amepitisha mwito unaothibitisha kwamba Liberia inastahili kupokea msaada wa fedha za maendeleo kutoka Mfuko wa UM juu ya Ujenzi wa Amani. Kadhalika KM ameliamrisha Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Liberia (UNMIL) lianze kushauriana na wenye madaraka Liberia pamoja na mashirika ya kiraia na kuandaa ni miradi gani itafaa kupewa umbele katika kupokea misaada hiyo ya UM.