Majadiliano ya ya kidiplomasiya ndio hatua ya kukomesha vurugu la Darfur, kunasihi Sudan
Kwenye mjadala wa wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu la UM, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Lam Akol alinasiihi kwenye risala yake ya kuwa majadiliano ya kidiplomasiya ndio njia pekee iliosalia kutumiwa na jumuia ya kimataifa yenye uwezo wa kukomesha vurugu la Darfur.
Akol alisema Serekali yake imejiandaa kushiriki kikamilifu kwenye majadiliano ya amani yatakayofanyika baadaye mwezi Oktoba nchini Libya, na alipendekeza pia kwa makundi yote ya waasi kukomesha, halan, uhasama na kujiunga na mazungumzo haya ya amani.