Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la saratani Tanzania na juhudi za kimataifa kukabiliana na usumbufu huu wa afya

Tatizo la saratani Tanzania na juhudi za kimataifa kukabiliana na usumbufu huu wa afya

Kwa kufuatana na taarifa za UM kuhusu maradhi hatari duniani imethibitishwa ugonjwa wa saratani ni miongoni mwa maradhi mazito ambayo bado yanaendelea kusumbua umma wa kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti, saratani kila mwaka husababisha idadi kubwa ya vifo kushinda maradhi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria yakijumlishwa pamoja.

Hospitali ya Ocean Road mjini Dar es Salaam, Tanzania ni taasisi pekee nchini yenye fursa na vifaa vya kisasa kuhudumia wagonjwa wa saratani. Hivi karibuni nilifanya ziara ya kituo hicho cha afya na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Hospitali ya Ocean Road, Daktari Twalib Ngoma.

Kwa mahojiano kamili sikiliza idhaa ya mtandao.