WFP kuhudumia chakula watu milioni 2 Sudan ya kusini kwa 2007
Shirika la WFP limeripoti kwamba litashiriki kwenye mpango wa kimataifa wa kuwahudumia chakula watu milioni 2 muhitaji waliopo Sudan ya kusini katika mwaka 2007.
Shirika la WFP limeripoti kwamba litashiriki kwenye mpango wa kimataifa wa kuwahudumia chakula watu milioni 2 muhitaji waliopo Sudan ya kusini katika mwaka 2007.
Mjumbe Maalumu wa UM kwa Darfur, Jan Eliasson wa Usweden anatazamiwa kukamilisha ziara yake rasmi katika Sudan wiki hii. Alifanikiwa kuonana kwa mazungumzo na viongozi kadha wa kadha wa Serekali ya Sudan na pia wale wanaowakilisha makundi ya waasi waliotia sahihi Maafikiano ya Abuja na wale wasioridhia itifaki hiyo.
Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kufumka kwa mapigano ya kikabila hivi majuzi katika eneo la Chad ya kusini karibu na jimbo la magharibi la Sudan la Darfur, hali ambayo inasemekena ilisababisha raia 20,000 wa Chad kung\'olewa makazi mnamo wiki tatu zilizopita.
Januari 01, 2007 Ban Ki-moon, aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Jamhuri ya Korea au Korea ya Kusini, alianza kazi rasmi kama ni KM wa nane wa Umoja wa Mataifa.
KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa maalumu iliyoyahimiza makundi yanayohasimiana Usomali kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukomesha, halan, vitendo vyote vya umwagaji damu.”
Kikao cha awali kwa mwaka 2007 cha Baraza kilikutana mwanzo wa wiki na wajumbe wanaowakilisha mataifa 15 wanachama waliratibu ajenda iliyoyapa umuhimu masuala yanayoambatana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Cote d’Ivoire, Mashariki ya Kati pamoja na vitisho vya jumla dhidi ya amani ya kimataifa.
Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuanzishwa tena zile huduma za kupeleka misaada ya chakula kwenye maeneo ya Usomali yaliyoathirika na mafuriko, baada ya shughuli hizo kusimamishwa kwa muda pale mapigano yalipofumka katika wiki zilizopita.
Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameripoti wasiwasi wake juu ya usalama wa wahamiaji wa Usomali wanaokimbilia Kenya.
Shirika la UM juu ya Huduma za Amani katika Sudan (UNMIS)limethibitisha kwenye ripoti iliyotoka majuzi kwamba wanajeshi wanne wa Bangladesh, waliotuhumiwa makosa ya kijinsiya katika eneo la Juba, Sudan walilazimika kurejeshwa makwao miezi michache iliopita.
Wanajeshi wa UM juu ya ulinzi wa amani nchini Burundi walifunga shughuli zao mnamo tarehe 31 Disemba 2006.