Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masuala kuhusu DRC, Mashariki ya Kati na Cote d'Ivoire kutawala ajenda ya Baraza la Usalama katika Januari

Masuala kuhusu DRC, Mashariki ya Kati na Cote d'Ivoire kutawala ajenda ya Baraza la Usalama katika Januari

Kikao cha awali kwa mwaka 2007 cha Baraza kilikutana mwanzo wa wiki na wajumbe wanaowakilisha mataifa 15 wanachama waliratibu ajenda iliyoyapa umuhimu masuala yanayoambatana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Cote d’Ivoire, Mashariki ya Kati pamoja na vitisho vya jumla dhidi ya amani ya kimataifa.