Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yarudisha tena huduma za kiutu Usomali kwenye maeneo ya mafuriko

WFP yarudisha tena huduma za kiutu Usomali kwenye maeneo ya mafuriko

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuanzishwa tena zile huduma za kupeleka misaada ya chakula kwenye maeneo ya Usomali yaliyoathirika na mafuriko, baada ya shughuli hizo kusimamishwa kwa muda pale mapigano yalipofumka katika wiki zilizopita.