FAO yawakutanisha wakulima wa mpunga Tanzania kuangalia sera na masoko
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake watafiti wa mpunga, Tari na IIRI wamewakutanisha baadhi ya wakulima wa mpunga nchini humo wapeane mawazo jinsi ya kuboresha zao hilo ili pamoja na faida nyingine, waweze kuhudumia soko la nchi zinazoizunguka Tanzania.