Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vipimo vya VVU vyapungua UNITAID waomba ufadhili zaidi

Vipimo vya virusi vya ukimwi.
Public Health Alliance/Ukraine
Vipimo vya virusi vya ukimwi.

Vipimo vya VVU vyapungua UNITAID waomba ufadhili zaidi

Afya

Kuelekea kilele cha siku ya UKIMWI Duniani Desemba 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limesema usumbufu na ucheleweshaji wa huduma za VVU unaosababishwa na janga la COVID-19 ulisababisha kupungua kwa vifaa vya upimaji na utambuzi wa VVU kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana ndani ya miongo miwili.

Huko ALIMA nchini COTE D’IVOIRE katika kituo cha zahanati anaonekaa muuguzi kwenye video ya UNITAID akielezea jinsi ya kutumia vifaa vya kujipima Virusi vya Ukimwi VVU, kisha wananchi hao hupewa vifaa hivyo na kwenda kujipima wenyewe nyumbani. 

Lakini Msemaji wa UNITAID Hervé Verhoosel, anasema baada ya janga la COVID-19 hali imebadilika na vipimo hivyo vimepungua sana ikilinganishwa na miongo miwili iliyopita. "Kuelekea Siku ya UKIMWI Duniani, Desemba 1, UNITAID inatoa wito kwa wafadhili kuongeza ufadhili wa haraka kwenye vifaa vya upimaji wa Virusi Vya Ukimwi VVU ili kulinda maendeleo yaliyodhoofishwa na COVID-19 na njia salama ya kuzuia VVU kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.”

Takwimu zilizokusanywa kwa pamoja, UNITAID na WHO zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2015 na 2020, idadi ya nchi zilizo na sera za kujipimaVVU imeongezeka kutoka mataifa sita hadi 88 - na mataifa mengine 31 yanaandaa será hizo". 

Kujipima VVU kumesaidia kufikia idadi ya watu wakiwemo wanaume na vijana ambao wana uwezekano mdogo wa kufikia vituo vya afya na walikuwa na viwango vya chini vya upimaji na walengwa wakuu wanaolengwa kutumia vifaa hivyo ni wale ambao kusita kutembelea vituo vya afya kwa sababu ya unyanyapaa au ubaguzi, kama anavyoeleza Mkurugenzi Mkuu wa UNITAID Dkt  

“Vifaa ni muhimu sana, lakini vifaa ambavyo watu wanaweza kutumia peke yao ni muhimu zaidi sasa na hali ya COVID-19, kwa sababu imekuwa ngumu zaidi kwenda hospitali na vituo vya afya. Kwa Vifaa  kama vile kujipima VVU , tumeona kabla ya COVID-19 kwamba tunaweza kufikia watu ambao hawana uwezo wa kufikia vipimo. Katika hali hii, kujipima mwenyewe ni muhimu kabisa, kwa sababu ni hatua ya kwanza kuelekea kupata matibabu.”