Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Watu binafsi pamoja na mashirika wanahakikisha watoto wanazingatia unawaji mikono kwa mfano mama na mwana Kenya
© UNICEF/Translieu/Nyaberi

Maimam wa Garissa nchini Kenya na UNICEF wasongesha chanjo ya COVID-19

Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kutikisa dunia huku taarifa potofu kuhusu chanjo zikiendelea kusambaa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo na faida zake katika kuepusha kusambaa zaidi kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. Taarifa ya John Kibego inafafanua zaidi.

Sauti
2'12"
Mabinti wakiwa wametoka kuteka maji
© UNICEF/Scott Moncrieff

Vyanzo vya maji zamani havikukauka kama sasa, jua ni Kali mno- Mfugaji 

Umoja wa Mataifa ukiendelea kutaka hatua zaidi kwa ajili ya tabianchi kama njia mojawapo ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania madhara hayo yako dhahiri kwa wafugaji wa wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ambao kupitia taarifa hii iliyoandaliwa na Mathias Tooko wa Radio washirika Loliondo FM wanaeleza hali ilivyokuwa zamani na sasa. 

Sauti
1'54"
Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA limezindua kampeni ya hakimiliki ya mwili kwa lengo la kuelimisha juu ya ukatili wa kijinsia mtandaoni hususan dhidi ya wanawake na wasichana na kutaka hatua zichukuliwe kuukomesha
UNFPA

Hakimiliki ya mwili wa mwanamke ipewe uzito mtandaoni kama haki miliki zingine:UNFPA 

Kampeni mpya iliyozinduliwa mwezi huu wa Desemba na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani linalohusika pia na afya ya uzazi UNFPA ya “Hakimiliki ya miwli wa binadamu” ina lengo la kuwasukuma watunga sera, sekta za teknolojia na mitandao yote ya kijamii kuuchukulia unyanyasaji na ukatili wa miili ya binadamu hususani ya wanawake mtandaoni kuwa ni suala linalohitaji kupewa uzito kama ilivyo ukiukwaji wa hakimiliki zingine. Flora Nducha na taarifa kamili 

Sauti
2'3"
Samaki waliovuliwa kwenye shamba la samaki la familia kufuatia mfumo wa umwagiliaji unaovuta maji kutoka mto ulio jirani.
UN Photo/Logan Abassi

Mafunzo na fedha taslimu kutoka UNHCR vyarejesha tabasamu kwa wakimbizi Côte d’Ivoire

Nchini Cote d’Ivoire  shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta tabasamu na nuru kwa wakimbizi ambao biashara zao zilivurugika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambalo limetikisa dunia kuanzia mwaka jana wa 2020. Kwa sasa wakimbizi hao wakiwemo wa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wana imani ya kujiinua tena kiuchumi.

Sauti
2'39"
Daktari wa mifugo akimchunguza kuku mgonjwa.
FAO/Giulio Napolitano

Kutoka ukimbizi arejea nyumbani na kufuga kuku sasa ni mfano kwa wenzake Burundi

Kijana Evariste Niyonzima mkazi wa sasa wa viunga vya jiji la Bujumbura nchini Burundi aliporejea nchini mwake kutoka ukimbizini katika nchi jirani ya Tanzania, alikuwa na mawazo kuwa atakapomaliza tu masomo atapata ajira ya ofisini itakayompa kipato hadi pale alipogundua kuwa hali halisi ni tofauti na alivyofikiria. Hata hivyo hivi sasa amefanikiwa kuliko hata baadhi walioajiriwa ofisini. Alifanyaje? Edwije EMERUSENGE ni mwandishi wa Televisheni washirika, Mashariki TV ya Burundi ameipata siri ya mafaniko anasimulia zaidi.

Sauti
2'35"
Vijana nchini Mali wakishiriki kwenye maigizo kama njia mojawapo ya kupaza sauti ya amani.
MINUSMA/Marco Dormino.

Sanaa na utamaduni vyatumika kuchagiza amani nchini Mali

Tofauti zinapaswa kuimarisha jamii badala ya kuisambaratisha, huo ndio  ujumbe uliotamalaki wakati wa kampeni iliyoendeshwa nchini Mali na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA kwa kushirikiana na chama cha wadau wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MANU. Kampeni ilileta pamoja wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume pamoja na Watoto wenye vipaji vya Sanaa na utamaduni.

Sauti
2'39"