Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

UN sasa kuwa na mashiko mashinani- Guterres

Baada ya mashauriano ya muda mrefu, hatimaye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeridhia mapendekezo ya marekebisho ya mfumo wa maendeleo wa chombo hicho chenye wanachama 193. Marekebisho hayo yanalenga kusogeza zaidi UN kwa wananchi wa kawaida ili hatimaye maendeleo yawe dhahiri ya watu na si vitu.

Audio Duration
4'3"
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore akiwa ziarani Mali
UNICEF/Keïta

Watoto zaidi ya milioni nchini Mali hawasomi

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore anazuru Mali ambako miaka sita baada ya kuanza mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo ghasia zinazidi kuongezeka huku watoto nao wazidi kunyimwa haki zao kama vile chakula, elimu na kuishi.

Picha ya UN News/Patrick Newman

Kazi ya Ulinzi wa amani ya UM imefikisha miaka 70.

 

Mwaka huu   Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 70 ya kuanza kazi rasmi hizo ambazo zimewahusisha wanaume na wanawake ambao wanatumwa sehemu mbalimbali na majukumu tofauti. Katika operesheni hizo 57 zimefanyika   tangu mwaka 1988. Pia operesheni nyingi zimetokea barani Afrika.

Walinda amani hao kila mmoja anaiona shughuli hiyo kivyake.Mmoja wa walinda amani wa kikosi hicho anaelezea jinsi kazi ilivyo. Siraj Kalyango  wa Idhaa hii amezungumza  nae na kuanza kujitambulish ni nani na anafanya kazi wapi.

Sauti
3'33"