Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda yaanzisha viza maalum ya kuchochea wahamiaji wenye ujuzi

iHub ni kituo cha ubunifu na biashara kupitia teknolojia nchini Kenya.
Picha: iHub/UNDP
iHub ni kituo cha ubunifu na biashara kupitia teknolojia nchini Kenya.

Rwanda yaanzisha viza maalum ya kuchochea wahamiaji wenye ujuzi

Ukuaji wa Kiuchumi

Nchi za Afrika sasa zaamka na zimeanza kujiwekea mifumo bora ya kisera ili uhamiaji uwe na matunda ndani  ya bara hilo.

Uhamiaji barani Afrika unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi endelevu na kuleta mabadiliko stahili ya kiuchumi kwa nchi husika iwapo kutakuwepo na mifumo bora ya kisera kuhusu uhamiaji.

Kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema hayo leo kwenye ripoti yake ya maendeleo barani Afrika,  ikiangazia zaidi marekebisho ya mfumo wa uhamiaji ili uwe na manufaa.

Ripoti hiyo pamoja na kuonyesha kuwa waafrika siyo tu wanakimbilia Ulaya bali pia wanahamia nchi nyingine za Afrika, imetaja mafanikio ya uhamiaji wa ndani Afrika uliochochewa na mifumo bora iliyowekwa na nchi za Afrika.

Mifano hiyo ni mingi lakini Jane Muthumbi, afisa wa UNCTAD, huko Geneva, Uswisi amezungumza na Idhaa hii na kutaja baadhi.

(Sauti ya Jane Muthumbi)

Ripoti hii inayoonyesha kuwa Afrika sasa nalo ni eneo ambako wahamiaji kutoka bara hilo wanahamia, ina lengo la kusaidia kuimarisha msimamo wa Afrika katika makubaliano ya kimataifa ya uhamiaji yanayotarajiwa kupitishwa mwezi disemba mwaka huu huko Marrakesh, Morocco.