Mchango wa Tanzania kwenye ulinzi wa amani ni dhahiri- Balozi Mahiga

29 Mei 2018

Nchini Tanzania nako maadhamisho ya siku ya walinda aman iwa Umoja wa Mataifa ambapo imeelezwa kuwa ni siku muhimu kwa kuzingatia kuwa katika miaka 70 ya ulinzi wa amani wa UN, Tanzania imeshiriki operesheni hizo kuanzia mwaka 2006. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema ingawa ni muda mfupi, mchango wa nchi hiyo umetambulika.

Balozi Mahiga akaenda mbali zaidi akisema..

Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza kuhusu kilichoamuliwa baada ya mauaji ya walinda Amani wa Tanzania huko Beni, Kivu Kaskazini nchini DR Congo mwaka jana, amesema, “Ilionekana kuwa usaidizi wa nyongeza utatolewa au utapaswa kutolewa ili kuepusha kile kilichotokea huko Beni tarehe 7 disemba mwaka jana na mashauriano hayo bado yanaendelea vizuri.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter