Je wanavijiji watamudu nishati mbadala ili kulinda misitu Tanzania?

Katika jitihada za pamoja za Umoja wa Mataifa na serikali duniani kuhakikisha misitu inalindwa ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imejiwekea mkakati kabambe wa miaka 5 kwenda sanjari na lengo hilo.
Hayo yameelezwa na Dk Ezekiel Mwakaluka ambaye ni mkurugenzi wa Misitu na nyuki katika wizara ya maliasili na utalii nchini tanzania alipohojiwa na idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York.
Akizungumzia changamoto ya uhifadhi wa misitu hususani kwa wananchi wa vijijini walio na kipato cha chini ambao kwa asimilia kubwa wanalazimika kutumia mkaa Dk Ezekiel alisema....
Na endapo serikali ina mpango wa kueneza umeme kuepusha hilo, wanavijiji wanawezeshwa vipi kumudu gharama za umeme, wakati mkaa na kuni wanapata bure ?