Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto zaidi ya milioni nchini Mali hawasomi

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore akiwa ziarani Mali
UNICEF/Keïta
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore akiwa ziarani Mali

Watoto zaidi ya milioni nchini Mali hawasomi

Afya

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore anazuru Mali ambako miaka sita baada ya kuanza mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo ghasia zinazidi kuongezeka huku watoto nao wazidi kunyimwa haki zao kama vile chakula, elimu na kuishi.

Bi. Fore katika ziara hiyo ameanzia kituo cha  afya cha Safo kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako ambapo wanawake wanapeleka watoto wao kupata huduma za kiafya wanazohitaji.

Hii ni kwa sababu zaidi ya watoto, 850,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo, huku wengine 274, 000 hali yao ni taabani.

Nayo maeneo ya kaskazini na kati mwa Mali yanakabiliwa na viwango vya juu zaidi vya utapiamlo kutokana na mapigano,sana sana karibu na eneo la Timbuktu, huko idadi ya watoto ni zaidi ya asilimia 15. 

“Watoto wa Mali kwa kweli wanateseka kimoyomoyo. Ni shida nchini Mali kwa sababu ya  kuongezeka kwa ghasia, lakini pia na umri nao umechangia. Kwa utapiamlo watoto wengi hawakuwa wanapata chakula wanachohitaji na tuna wasiwasi kuwa  zaidi ya robo milioni ya watoto watafariki dunia mwaka huu wakati wa mavuno madogo na hivyo ina maana kuwa kuna hofu na hofu hiyo ni kwa watoto wote.

Hatimaye Mkurugenzi Mtendaji huyu wa UNICEF alitembea moja ya darasa la shule ya watoto mjini Bamako.

Watoto wanaonekana na ari ya masomo, ingawa inaelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni moja nchini Mali hawasomi na idadi yao iliongezeka kwa asilimia 30 tangu mwaka wa 2009 ambapo watoto 637,000 waliripotiwa kukosa masomo.

Na ndipo Bi. Fore akafunguka kuhusu hali ya watoto aliyoshuhudia.

Bi Henrietta Fore akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kalabambougou, mjini BAMAKO, MALI anatarajiwa labda kuongezea dau kutokana na jinsi alivyoshudia hali ilivyo.

Hadi sasa shule 750 baado zimefungwa katika sehemu za kaskazini na katikati mwa nchi hiyo kutokana na hali za usalama ambazo zinaaathiri watoto zaidi ya 300,000 walio na umri wa kwenda shule.Wale ambao wako shuleni na baadhi kutembelewa na mkuu wa UNICEF walifurahi na kushangilia.

“Watoto hao pia hawako shuleni, kwa hivyo watoto zaidi milioni moja wanakosa elimu ya msingi na wengine milioni moja hawapati elimu ya sekondari.”