Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Ndani ya moja ya kituo cha wakimbizi wa ndani kwenye mji wa Bambari jimbo la Ouaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
OCHA/Gemma Cortes

Si kila kitu cha bure ni kibaya

Awali wananchi walipata shida kufika polisi ili kueleza madhila yao, lakini hivi sasa Umoja wa Mataifa umeweka mazingira ambamo kwayo wananchi wanaripoti polisi madhila yanayowakumba kwa urahisi na pia bila gharama yoyote.

Sauti
1'58"
Bidhaa kama hizo zinawafanya wanawake kujiendeleza
Picha ya IFAD/Santiago Albert Pons

Uchuuzaji mboga wanusuru wanawake dhidi ya umaskini Uganda

 Umoja wa Mataifa  unahimiza kuleta   maendeleo kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu SDGs.Mathalani   lengo namba moja la kutokomeza  umaskini kwa ifikapo mwaka wa 2030. Kwa mantiki hiyo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini .  Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango amevinjari eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wanawake hao na kutuandalia Makala ifuatayo.

Sauti
3'32"