Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misukosuko ya ardhi yetu yatukera- Endorois

Washiriki katika jukwaa la 17 la watu wa asili.
UN / Evan Schneider
Washiriki katika jukwaa la 17 la watu wa asili.

Misukosuko ya ardhi yetu yatukera- Endorois

Haki za binadamu

Jamii ya asili wanahaha kila uchao kuhakikisha kwamba wanapata haki yao ya msingi hususan ile ya ardhi. Jamii hii hukumbwa na misukosuko mingi hasa inapodai haki ya ardhi yao ya asili ambayo ina maana kubwa kwao kuliko inavyofikiriwa.

Jukwaa la watu wa jamii ya asili likiendelea jijini New  York, Marekani mshiriki kutoka Baringo nchini Kenya amesema wanakerwa na misukosuko wanayokumbana nayo wakati wanapopokwa maeneo yao ya ardhi.Siraj Kalyango na taarifa kamili.

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Carson Kiboro Kibeti kutoka jamii ya ENDOROIS inayopatikana sehemu za Baringo nchini Kenya akihojiwa nami kando ya mkutano huo alianza kwa kuelezea jamii ambayo anawakilisha katika jukwaa hili la jamii ya asili

(Carson Kiboro Kibeti )

Kama zilivyo jamii nyingine za asili duniani, wao nao wanataka waendelea kumiliki ardhi yao ya asili. Mbali na shida hiyo waENDOROIS wanakabiliwa na shida nyingine.

Watu wa jamii ya asili wanataka ardhi yao kwani ni zaidi ya kile ambacho watu wanafikiria
IIED- GEF Small Grants Programme, UNDP
Watu wa jamii ya asili wanataka ardhi yao kwani ni zaidi ya kile ambacho watu wanafikiria

(Carson Kiboro Kibeti )

Mwaka 1973 serikali ya Kenya iliwaondoa watu wa jamii hiyo kutoka maeneo yao na kutaka kukuza eneo hilo kuweka vivutio vya utalii.

Jamii hiyo  ililipinga na kwenda mahamakani ya Umoja wa Afrika nchini Gambia. Kibet amenieleza sababu ya kwenda mahakamani.

(Carson Kiboro Kibeti )