Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia unazidi kuimarika-IMF

Uvuvi ni moja wa nyanja zinazochangia ukuaji wa uchumi
Picha na Benki ya Dunia/John Hogg
Uvuvi ni moja wa nyanja zinazochangia ukuaji wa uchumi

Uchumi wa dunia unazidi kuimarika-IMF

Ukuaji wa Kiuchumi

Uchumi wa dunia unazidi kupanda taratibu licha ya matatizo ya hapa na pale, imesema ripoti mpya ya shirika la fedha duniani la IMF inayochunguza mwelekeo wa uchumi wa dunia

Mchumi mkuu wa shirika hilo la fedha duniani, IMF Maury Obstfed, amesema kuwa wanategemea uchumi kuendelea kukua.

(SAUTI YA MAURY OBSTFED)

“Ukuaji tulioshuhudia ulioanza katikati ya mwaka wa 2016 unaendelea. Baada ya ukuaji  wa mwaka jana wa asilimia 3.8, tunatarajia ukuaji wa asili mia 3.9 mwaka huu na mwaka ujao. "

Hata hivyo ripoti hiyo ya IMF inaonya kuwa maendeleo hayo yanaweza kutatizwa tu iwapo mataifa yataweka vikwazo vya kibiashara.

(SAUTI YA MAURY OBSTFED)

"Ujumbe muhimu kwa sasa ni kuwa msikubali mvutano kuhusu biashara uwavute watunga sera kutoka changamoto za muda mrefu za kuuweka uchumi kuwa imara zaidi na pia kuwa jumuishi. " 

Mchumi huyo pia ameonya dhidi ya athari za kupanda zaidi kwa kiwango cha deni ambacho amesema kuwa sasa ni cha juu zaidi tangu vita kuu ya pili vya dunia.

(SAUTI YA MAURY OBSTFED)

 “Pia tunashudia viwango vya madeni viko juu, likiwemo deni binafsi na hilo linaweza kuzusha wasiwasi wakati  huu ambapo sera za kifedha zinatengamaa na viwango vya riba vinapanda."