Si kila kitu cha bure ni kibaya

18 Aprili 2018

Awali wananchi walipata shida kufika polisi ili kueleza madhila yao, lakini hivi sasa Umoja wa Mataifa umeweka mazingira ambamo kwayo wananchi wanaripoti polisi madhila yanayowakumba kwa urahisi na pia bila gharama yoyote.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MINUSCA umechukua hatua kuhakikisha wanapunguza na hatimaye kutokomeza vitendo vya ukatili vinavyoenda sambamba na ukwepaji sheria. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Ndani ya kambi ya wakimbizi wa ndani kwenye mji wa Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wako kwenye doria huku wakimbizi wakiendelea na shughuli zao za kawaida.

Doria hii imeimarishwa tangu mwezi Januari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya MINUSCA ya kuhakikisha hakuna ukwepaji sheria kwa vitendo kama vile ubakaji, uporaji na mauaji vilivyokuwa vimeshamiri kwenye kambi za wakimbizi wa ndani zinazohifaji maelfu ya raia waliofurushwa makwao na vikundi vilivyojihami. Marie-Joseph Goueth ni polisi wa Umoja wa Mataifa ndani ya MINUSCA.

(Sauti ya Marie-Joseph Goueth)

"Baadhi ya malalamiko yamepata suluhuisho na mengine yako kwenye mchakato wa kisheria yakifuata utaratibu wa kawaida.”

Wakimbizi wa ndani wamepigia chepuo mpango huo kwani idadi ya visa vilivyoripotiwa polisi tangu kuanza kwa mchakato huo imeongezeka. Nina Keta-Kossi ni mkimbizi wa ndani.

(Sauti ya Nina Keta-Kossi)

"Mtu hatozwi fedha kwa kuandikisha malalamiko. Kila kitu ni bure. Iwapo mtu amefanya uhalifu, halii hii inahamasisha kutokomeza.”

Polisi jami na ulinzi shirikishi vimefanikisha mpango huu ambapo waratibu walio kambini ndio wanapokea malalamiko na kuwasilisha polisi. Ferdinant Patrice ISaa ni kamishna wa polisi.

(Sauti ya Kamishna Fernand Patrice Issa)

"Mpango wetu ni kutekeleza polisi jamii. Kwa hiyo katika vituo vyote vinavyozingira mji wa Bambari tunaelewana na wananchi kwa sababu raia wanapokuwa na shida au wako hatarini wanakimbilia polisi na sisi tunachukua hatua mara moja.”

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter