Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchuuzaji mboga wanusuru wanawake dhidi ya umaskini Uganda

Bidhaa kama hizo zinawafanya wanawake kujiendeleza
Picha ya IFAD/Santiago Albert Pons
Bidhaa kama hizo zinawafanya wanawake kujiendeleza

Uchuuzaji mboga wanusuru wanawake dhidi ya umaskini Uganda

Wanawake

 Umoja wa Mataifa  unahimiza kuleta   maendeleo kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu SDGs.Mathalani   lengo namba moja la kutokomeza  umaskini kwa ifikapo mwaka wa 2030. Kwa mantiki hiyo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini .  Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango amevinjari eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wanawake hao na kutuandalia Makala ifuatayo.

Ni  soko la kando la  mwa barabara likiuza matunda sanasana nyanya, pilipili- hoho na matunda mengine. Soko hili linaitwa Kakinga Farmers market na ni  wanawake pekee  ndio wanaohudumu mahali hapo.Mastura Nasimbwa ni mwenyekiti wa soko hilo , anasema kwanini ni jinsia moja tu inaloshughulika mahali hapo.

(SAUTI YA NASIMBWA)

“ Sababu wanaume ni wavivu hawawezi kufanya kazi kama hii ya kuuza nyanya na vitu vidogo kama hivi ni sisi tu wanawake ndio tunaweza kufanya kazi.

Aongeza kuwa katika soko hilo kuna wanawake 52 wanaoendesha biashara zao. Mmoja wao ni Mama Hajara asema biashara inakwenda taratibu.

(SAUTI YA MAMA HAJARA1)

Mama Hajara anaendelea kuwa kawaida kila box moja la nyanya mbichi hulinunua shillingi ambazo ni sawa na dola 50.  Mama huyu mjasilia mali anafafanua.

(SAUTI YA MAMA HAJARA2)

Bila shaka biashara ya matunda upande mwingine  huleta hasara kama vile matunda kuoza . Je! tatizo hilo nalo linawakumba la nyanya kuoza?

(SAUTI YA MAMA HAJARA3)

 Mbali na shida hiyo  ya  kuoza Mama huyu asema kuna matatizo mengine yanayomkera katika kazi yake hiyo.

(SAUTI YA MAMA HAJARA4)

 Akina mama hawa wajasiliamali wanajitahidi kuendeleza biashara zao lakini wanadumazwa na matatizo mbali mbali. Na wanasema wakiwezeshwa  watasonga mbele zaidi.

(SAUTI YA MAMA HAJARA5)

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo.. asema wangetaka wasaidiwe ili wapanue mahala pa kuegeshea magari kwa wateja wao ili waweze kununua biashara zao, katika soko ambalo liko kando ya barabara kuu itokayo Kampala kuelekea magharibi mwa nchi hiyo ikipitia Masaka.