Uwekezaji katika kilimo utawakomboa Wasyria:FAO
Uwekezaji katika kilimo umeelezwa kuwa ni muhimu sana na ndio utaokoa mustakhbali wa mamilioni ya Wasyria.
Uwekezaji katika kilimo umeelezwa kuwa ni muhimu sana na ndio utaokoa mustakhbali wa mamilioni ya Wasyria.
Kwa mara ya kwanza katika muongo mmoja uliopita hatua za kuelekea kutokomeza malaria zimekwaa kisiki na mafanikio yaliyopatikana yakishuhudiwa kubadili mwelekeo katika baadhi ya nchi kote duniani.
Hoja za nini kifanyike ili kuepusha mizozo na badala yake kuweka mazingira ya ujenzi wa amani endelevu zimewasilishwa hii leo kwenye Umoja wa Mataifa wakati wa kikao cha ngazi ya juu kilichoandaliwa na Baraza Kuu la umoja huo.
Mkutano wa siku mbili wa kuchangisha fedha kusaidia Syria umeanza leo huko Brussels, Ubelgiji, wakati huu ambapo kuna ripoti ya kwamab maeneo yaliyokuwa yanazingirwa sasa yanafikika.
“Ofisi yetu bado inajitahidi kukusanya taarifa kuhusu majina, umri na jinsia ya raia waliouawa na kujeruhiwa wakati wa tukio hilo la kikatili." Asema Liz Throssel wa Umoja wa Mataifa.
Wakati jukwaa la kimataifa la watu wa asili likiwa katika wiki ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, watu wa asili kutoka jamii ya Ogiek nchini Kenya wanasema wanakimbiza treni ya SDGs lakini bila mkono wa serikali kuikamata itakuwa mtihani.
Wanasema mchezea kwao hutunzwa, nae Mahmoud Abu Zeid, kwa jina la kupanga Shawkan, na raia wa Misri licha kuwa kizuizini amechaguliwa kuwa mshindi wa mwaka huu wa tuzo la uhuru wa uandishi habari laUNESCO/Guillermo Cano Press Freedom.
Jayathma Wickramanayake kutoka Sri Lanka amesema sasa vijana siyo tena kundi la ziada kwenye masuala ya amani na usalama, bali ni kundi muhimu zaidi katika kufanikisha ajenda hiyo.
Kamishina mkuu wa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amewasili Ethiopia kwa ziara ya siku nne ambapo atakutana na maafisa wa serikali lakini pia kushiriki mkutano wa ngazi ya juu wa Muungano wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa.
Nchini Uswisi, kampuni moja imeibuka na mbinu ya aina yake ya kutumia ushoni kama njia ya kujumuisha wakimbizi kwenye jamii.