Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maeneo yote sasa Syria yanafikika- WFP

Ghouta Mashariki , mtoto akipimwa na muhudumu wa afya ili kubaini endapo ana utapia mlo.
@UNICEF/UN/Tom/OCHA
Ghouta Mashariki , mtoto akipimwa na muhudumu wa afya ili kubaini endapo ana utapia mlo.

Maeneo yote sasa Syria yanafikika- WFP

Msaada wa Kibinadamu

Mkutano wa siku mbili wa kuchangisha fedha kusaidia Syria umeanza leo huko Brussels, Ubelgiji, wakati huu ambapo kuna ripoti ya kwamab maeneo yaliyokuwa yanazingirwa sasa yanafikika. 

Mkutano huo wa siku mbili unafanyika wakati zaidi ya watu milioni 13 nchini humo wanahitaji misaada ya kibinadamu ambapo nusu ya hao hawana uhakika wa chakula, baada ya vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 7 sasa.

Umoja wa Mataifa na wadau wakisaka fedha, shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema angalau hivi sasa majimbo yote 14 nchini Syria yakiwemo Raqqa na Deir-ez-Zour, [DER-A-ZUR] yanafikika baada ya magaidi wa ISIL waliokuwa wanazingira baadhi ya maeneo kufurumushwa.

Mkurugenzi mkazi wa WFP nchini Syria, Jakob Kern akizungumza huko Geneva, Uswisi kuhusu operesheni hizo za kusambaza chakula nchini Syria amesema wananchi wamefurahishwa sana kuona misaada inafika.

(Sauti ya Jakob Kern)

“Ghouta Mashariki hivi sasa haizingirwi tena, tumeweza kupata uwezo wa kuingia angalau na tunasaidia watu kupitia chama cha msalaba na hilal nyekundu cha Syria. Pia tunasaidia watu 150,000 waliokimbia mapigano wiki chache zilizopita. Watu 45,000 bado wanaishi kwenye makazi ya muda.”

Kwa mantiki hiyo amesema..

(Sauti ya Jakob Kern)

“Kwa sasa hakuna eneo lolote lililosalia limezingirwa nchini Syria. Hali ilivyo ni kwamba sasa tunaweza kufikia majimbo yote 14 nchini Syria.”