Uwekezaji katika kilimo utawakomboa Wasyria:FAO

25 Aprili 2018

Uwekezaji katika kilimo umeelezwa kuwa ni muhimu sana na ndio utaokoa mustakhbali wa mamilioni ya Wasyria.  

Hayo yamesemwa hii leo na shirika la chakula na kilimo FAO mjini Brussels Ubeligiji kwenye mkutano wa kimataifa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu wa Syria.

Nchi hiyo ambayo imeghubikwa na vita kwa zaidi ya miaka saba sasa kwa asilimia kubwa vita hivyo vimejikita katika maeneo muhimu ya kilimo na kuathiri sekta hiyo vibaya sana.

FAO inasema hasara katika sekta ya kilimo Syria inakadiriwa kuzidi dola bilioni 16 kutokana na wakulima kutawanywa, miundombonu kusambaratika na mifugo kupotea, hali iliyopunguza uzalishaji kwa kiasi kikubwa na kupandisha bei ya chakula. Dominique Burgeon ni mkurugenzi wa FAO idara ya mipango na dharura

(SAUTI YA DOMINIQUE BURGEON)

“Kilimo Syri wakati wote kimekuwa na jukumu kubwa , kabla ya vita kuanza kilikuwa moja ya sekta muhimu kwa uchumi wa Syria kikichangia asilimia 18 ya pato la ndani la taifa, kilikuwa kinatoa fursa za ajira kwa asilimia 17 ya ajira zote, kikichangia usafirishaji bidhaa nje na kilikuwa ndicho kinalisha watu w anchi hiyo.”

FAO imezisihi nchi zinazohudhuria mkutano huo kuwekeza katika kilimo Syria kama njia itakayosaidia kurejesha utulivu na ujenzi mpya wa taifa hilo.  Pia imechagiza kushughulikia mizizi iliyochangia mgogoro wa Syria kuwa janga kubwa la kibinadamu.

Kwas asa shirika hilo linahitaji dola milioni 120 kwa ajili ya mipango ya kuisaidia Syria kwa mawaka 2018 , lakini hadi sasa imepata robot u ya kiwango hicho.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter