Ushoni waleta nuru kwa wakimbizi Uswisi

23 Aprili 2018

Nchini Uswisi, kampuni moja imeibuka na mbinu ya aina yake ya kutumia ushoni kama njia ya kujumuisha wakimbizi kwenye jamii. 

Katika karakana hii ya ushonajiwa nguo mjini Zurich, Heather Kirk ambaye ni mwanabayologia, ametumia udadisi wake maendeleo endelevu na kazi ya kijamii kuleta pamoja wakimbizi kupitia kampuni yake ya Social Fabric.

Kila siku ya alhamisi, wakimbizi kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Afghanistan hufika katika karakana hii na kujifunza bila gharama yoyote ushonaji wa nguo.

Bi. Kirk anasema kwa kuwa lugha inayozungumzwa kijerumani, wakimbizi nao wanajikuta wanajifunga lugha hiyo na hivyo kurahasisha utengamano katika jamii.

 (Sauti ya Heather Kirk)

“Ni vigumu sana kwa watu kujitegemea au kujiendeleza kielimu au hata kuajiriwa pindi wakiwa ni wakimbizi. Kwa hiyo inabidi tuwe wabunifu zaidi tunapofikiria jinsi ya kusaidia utangamano.”

Baada ya kupata mafunzo, wakimbizi hao nao hujitolea kushona nguo hizo na fedha zinazopatikana

Nats..

Huyu ni Cisse mmoja wa wanafuika na tayari amekamilisha kushona shati na amelijaribu akiuliza iwapo limekaa sawa na anajibiwa kuwa liko sawa !

Nats..

Zaidi ya wakimbizi 80 wamenufaika na mafunzo hayo na hivyo kuwapatia fursa bora zaidi ya kuajiriwa nchini Uswisi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter