Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waogiek tunajikongoja Kenya,serikali tushikeni mkono: Prengei

Washiriki wa jukwaa la 17 la watu wa jamii ya asili
UN / Evan Schneider
Washiriki wa jukwaa la 17 la watu wa jamii ya asili

Waogiek tunajikongoja Kenya,serikali tushikeni mkono: Prengei

Utamaduni na Elimu

Wakati jukwaa la kimataifa la watu wa asili likiwa katika wiki ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, watu wa asili kutoka jamii ya Ogiek nchini Kenya wanasema wanakimbiza treni ya SDGs lakini bila mkono wa serikali kuikamata itakuwa mtihani. 

Jamii ya Oginek ambayo ni miongoni mwa jamii za siku nyingi za watu wa asili nchini Kenya , tangu taifa hilo la afrika ya Mashariki kunyakua uhuru wake 1963, haikuwahi kuwa na seneta yeyote wa kufikisha sauti zao kwenye serikali haki sasa ambapo  PRENGEI VICTOR  ameingia katika historia ya jamii hiyo kuvaa viatu hivyo vya kwanza kwa jamii ya Ogiek.
Akizungumza na UN News amesema kuna changamoto nyingo zinazoikabili jamii yake lakini kwanza anaeleza majukumu yake katika baraza la seneti ya Kenya.

(SAUTI YA PRENGEI1)  

Prengei anasema anaamini hakuna lisilowezekana ingawa kila safari ni hatua. Kilio chake kwa serikali ya Kenya ni kuishika mkono jamii hiyo iliyoachwa na treni ya maendeleo hususan ya SDGs, kwani kwao muda unawatupa mkono kwa sababu,

(SAUTI YA PRENGEI2)
Ameongeza kuwa hawataki kupigwa jeki huko kuwe ni upendeleo bali ziwe ni njia za kuwawezesha mfano

(SAUTI YA PRENGEI 3)