Uteketezaji wa Rohingya unaendelea Myanmar:Gilmour
Uteketezaji wa watu wa kabila la Rohingya bado unaendelea nchini Myanmar , amesema msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Martaifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Andrew Gilmour.
Uteketezaji wa watu wa kabila la Rohingya bado unaendelea nchini Myanmar , amesema msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Martaifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Andrew Gilmour.
Leo ni siku ya wanyama pori duniani ambapo Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali likiwemo la Mazingira UNEP na CITES wanahimiza jamii kuhakikisha wanalinda wanyama pori hususani jamii ya paka wakubwa kama simba, chui, duma, puma na jamii yao kwani wako hatarini kutoweka.
Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa mgogoro wa Syria kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2401 la usitishwaji wa mapigano kwa siku 30 katika eneo la Ghouta mashariki nchini Syria na mji mkuu Damascas, ili kupisha misaada ya kibinadamu.
Mataifa yanayoendelea yameshauriwa, miongoni mwa mambo mengine, kuwawezesha vijana na pia kuhakikisha usawa wa kijinsia ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.
Wakazi wa Gazi na Makongeni huko Kwale mjini Mombasa nchini Kenya waliamua kushikamana na kulivalia njuga suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuanzisha mradi ambao pia unawakwamua katika umasikini.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema haba na haba hujaza kibaba kwa wakimbizi, hususani ambao sasa wamepata maskani ya kudumua na kuanza kujenga upya maisha yao kama binti sandrine kutoka Burundi.Siraj Kalyango anatupasha zaidi
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo tunaanzia huko DR Congo, ukiukwaji wa haki za binadamu wafurutu ada.
Nchini Uganda, milipuko ya homa ya Kongo na Bonde la Ufa yarejea.
Hatimaye vuta nikuvute ya uchaguzi nchini Liberia imefikia ukingoni baada ya mshindi aliyepatikana sasa kuapishwa rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo. Naye si mwingine bali ni George Weah, msakata kabumbu wa kimataifa ambaye sasa ametundika daluga na kujikita katika siasa.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yana fursa kubwa ya kuchagiza mchakato wa utekelezaji wa maalengo ya maendeleo endelevu au SDGs endapo changamoto zake zitashughulikiwa ipasavyo.