Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uteketezaji wa Rohingya unaendelea Myanmar:Gilmour

Maelfu ya watoto wakimbizi wa Rohingya wapanga foleni kupokea chakula cha msaada.
© UNICEF/UN0147302/Brown
Maelfu ya watoto wakimbizi wa Rohingya wapanga foleni kupokea chakula cha msaada.

Uteketezaji wa Rohingya unaendelea Myanmar:Gilmour

Amani na Usalama

Uteketezaji wa watu wa kabila la Rohingya bado unaendelea nchini Myanmar , amesema msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Martaifa  kuhusu masuala ya haki za binadamu Andrew Gilmour.

Gilmour ameyasema hayo leo mjini Cox’s Bazar nchini Bangladesh alipokuwa akihitimisha ziara yake baada ya kuzungumza na wakimbizi wa Rohingya walioko makambini.

UN News Kiswahili
Uteketezaji wa Rohingya unaendelea Myanmar:Gilmour

Baadhi ya wakimbizi aliowahoji wameelezea kuendelea kwa kiwango kikubwa cha mauaji, ukatili wa kingono, utesaji, ubakaji, kutekwa pamoja na kulazimishwa kukaa bila kula.

Bwana Gilmour amesisitiza ukweli kwamba si haki kutegemea wakimbizi hao kurejea Myanmar hivi sasa.

Wakati huohuo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hii leo limeonya kwamba hatari ya Wanyama pori inaongeza changamoto ya kuwasaidia wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh.

Alama barabarani ikionyesha mahali ndovu hupitia kambini Kutupalong na kituo cha UNHCR cha mpito Cox's Bazar
© UNHCR/Roger Arnold
Alama barabarani ikionyesha mahali ndovu hupitia kambini Kutupalong na kituo cha UNHCR cha mpito Cox's Bazar

UNHCR inasema eneo ambalo lina makazi ya wakimbizi ya Kutupalong mjini Cox’s Bazar, kwa muda mrefu yalikuwa ni maskani ya tembo wa Asia Mashariki.

Kuna takribani tembo 40 ambao wanasafiri kati ya Bangladesh na Myanmar kusaka chakula. Na kwa bahatii mbaya hadi sasa wakimbizi 10 wameuawa na tembo hkatika mkakazi hayo, watu wengine kujeruhiwa na pia kupoteza kila kitu.