Baraza la Usalama: mapigano kukoma kwa siku 30 Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2401 la usitishwaji wa mapigano kwa siku 30 katika eneo la Ghouta mashariki nchini Syria na mji mkuu Damascas, ili kupisha misaada ya kibinadamu.
Azimio hilo limetipitshwa baada ya vuta nikuvute kati ya baadhi ya nchi wanachama ikiwemo Urusi, Iran na Uturuki. Balozi Mansour Al-Otaibi ambaye ni rais wa Balaza la Usalama mwezi huu, amesema usitishwaji wa mapigano kwa siku 30, kupitia azimio hilo ,utayapa mashirika ya kibinadamu fursa ya kutoa misaada kwa mamilioni ya wakimbizi kutoka Syria na Palestina ambao milioni sita kati yao, wamehamiswa ndani Syria , na milioni 2.5 wakiishi katika maeneo hatarishi yaliozingizwa katikati ya mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa kundi linalodai ukombozi wa Syria na majeshi ya serikali.
Naye balozi Nikki Haley ambaye ni muakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa akizungumza katika mkutano huo amesema anashukuru jitihada za rais wa baraza la Usalama Bw. Monsour Al Otaibi katika kuhakikisha azimio la usitihswaji mapigano linapitishwa ili kuokoa maisha wa waathiria katika mgogoro wa Syria.
Baraza la Usalama limetoa wito kwa pande zote katika mgogoro wa Syria kuheshimu na kutekeleza azmio lililopitishwa na pia limewaomba wawakilishi wa nchi wanachama kutumia ushawishi wao ili kuweza kukomesha mapigano yanayoendela mashariki mwa Ghouta na kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi wanaohitaji huduma za kibinadamu.