Penye nia pana njia- Mikoko Pamoja
Tabianchi na mazingira
Wakazi wa Gazi na Makongeni huko Kwale mjini Mombasa nchini Kenya waliamua kushikamana na kulivalia njuga suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuanzisha mradi ambao pia unawakwamua katika umasikini.
Mradi huo ujulikanao kama "Mikoko Pamoja" ni wa kwanza kuendeshwa na jamii barani Afrika na umejikita katika upandaji wa mikoko ambayo inatoa hewa ya ukaa.
Wana mradi wanaikusanya na kuiuza katika makampuni na watu binafsi na fedha wanazopata zinawanufaisha wanajamii. Miongoni mwa wana mradi hao ni Bi Hafsa Mohamed Zuga na bwana Josephat Mwamba Mtwana walipata fursa ya kuzumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kuhusu mradi wao