Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya wanyama pori duniani:UN

Simba anaangalia mazingira yake nchini Kenya.
Photo: UN/DPI Photo
Simba anaangalia mazingira yake nchini Kenya.

Leo ni siku ya wanyama pori duniani:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya wanyama pori duniani ambapo Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali likiwemo la Mazingira UNEP na CITES wanahimiza jamii kuhakikisha wanalinda wanyama pori hususani jamii ya paka wakubwa kama simba, chui, duma, puma na jamii yao kwani wako hatarini kutoweka.

Pia kwa kushirikiana na muungano wa kimataifa wa kuhifadhi mali asili IUCN na taasisi ya kimataifa kuhusu mazingira na maendeleo IIED wamezindua ripoti na kutoa mapendekezo ya kuchukua hatua madhubuti kulinda wanyama pori.

Kwa pamoja wametaka jamii za watu wa asili zishirikishwe na pia jamii zote kwa ujumla katika vita dhidi ya uhalifu kwa wanyama pori ikiwemo ujangili na biashara haramu kama ya ngozi za chui. 

Wamesisitiza kuwa ni muhimu sana kwa jamii kulinda wanyama pori hususani walio katika hatari ya kutoweka kama jamii ya paka wakubwa.