UNICEF imetuepusha na maji yenye wadudu- Wakazi wa Cibitoke
Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa wiki ya maji duniani , nchini Burundi mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa serikali ya Japan umesaidia wakazi wa eneo la Cibitoke nchini Cibitoke siyo tu kuondokana na unywaji wa maji machafu yenye wadudu, bali pia kuepusha watoto dhidi ya magonjwa na watoto wa shule kuondokana na zahma ya kutembea muda mrefu kwenda kuteka maji badala ya kwenda shuleni.