Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chondechonde mamlaka Tigray rejesheni mafuta ya WFP yaliyoibwa:Beasley

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanachua hatua kusaidia makumi ya maelfu ya wakimbizi waliokimbia eneo la Tigray nchini Ethiopia na kuingia Sudan.
© WFP/Leni Kinzli
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanachua hatua kusaidia makumi ya maelfu ya wakimbizi waliokimbia eneo la Tigray nchini Ethiopia na kuingia Sudan.

Chondechonde mamlaka Tigray rejesheni mafuta ya WFP yaliyoibwa:Beasley

Msaada wa Kibinadamu

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ameitaka mamlaka ya Tigrayan kurejesha mara moja akiba ya mafuta iliyoibiwa kwa jumuiya ya kibinadamu.  

David Beasley amesema jana Jumatano asubuhi, kundi la watu wenye silaha waliingia katika ghala la WFP huko Mekelle na kukamata kwa nguvu meli 12 zilizojaa zaidi ya lita nusu milioni za mafuta. 

Amesisitiza kuwa “Mafuta haya yalikuwa yamenunuliwa na WFP hivi majuzi na yalifika siku chache kabla ya kuibwa. Bila mafuta hayo haiwezekani kwa WFP kusambaza chakula, mbolea, madawa na vifaa vingine vya dharura kote Tigray,” Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mamilioni ya watu watasukumwa zaidi kwenye njaa kwa kuzuka tena mapigano Kaskazini. Ethiopia. 

 Katika miezi michache iliyopita, makubaliano ya kibinadamu yameruhusu WFP na washirika wake kufikia karibu watu milioni 5 huko Tigray.  

Hata hivyo, jana njia hiyo ya kuokoa maisha ilikatwa, Bwana Beasley amesema, na kuongeza kuwa "Pia tukio hilo linatuzuia kuwasha jenereta na magari, ili WFP na washirika wa kibinadamu waweze kukidhi mahitaji ya watu wa Tigray wanaoishi katika mazingira magumu, ambapo wastani wa watu milioni 5.2 wanakabiliwa na njaa kali. Kupotea kwa mafuta haya kutasukuma jamii za Tigray, ambazo tayari zinakabiliwa na athari za vita, kuelekea kwenye ukingo wa njaa. "