Ulimwengu lazima 'ubadilishe mkondo' ili kulinda bahari dhidi ya janga la tabianchi - Guterres
Sayari dunia inakabiliwa na matatizo mara tatu ya uharibifu wa tabianchi, upotevu wa baionuai na uchafuzi wa mazingira, Katibu Mkuu António Guterres ameuambia Mkutano wa Bahari Moja #OneOceanSummit hii leo akionya kwamba, "bahari inabeba mzigo mkubwa".