Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kukomeshwa kwa mzozo wa Ethiopia  

Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina Mohammed na Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia walikutana na watu wa Somali ambao wanakabiliwa na majanga yanayosababishwa na ukame.
UNECA/Daniel Getachaw
Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina Mohammed na Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia walikutana na watu wa Somali ambao wanakabiliwa na majanga yanayosababishwa na ukame.

Naibu Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kukomeshwa kwa mzozo wa Ethiopia  

Amani na Usalama

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed aliyekuwa ziarani nchini Ethiopia na kutembelra eneo la Tigray kaskazini mwa nchini na maeneo mengine yenye migogoro, akihitimisha zaiara amesema safari ilikuwa ishara ya mshikamano na Waethiopia wote na akatoa wito wa kutamatisha mgogoro katika nchi hiyo ya barani Afrika. 

Ratiba yake ilianzia katika Mkutano wa Wakuu wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa wiki iliyopita. 

Matumaini 

Naibu Katibu Mkuu Amina J Mohammed amesema kuwa alipata heshima ya kufungua mkutano huo kwa kumwakilisha Katibu Mkuu, Antonio Guterres na kwamba alijadili mada kama vile migogoro ya kibinadamu na maendeleo. 

Lakini hasa kuhusiana na Ethiopia, amefichua kwamba alishuhudia janga la mzozo huo na akakumbuka kuwa katika hali hii kamwe hakuna mshindi. 

Akiwa anatembelea mikoa ya Tigray, Amhara na Somali, amesema kuwa ameona juhudi za serikali na watu kwa ajili ya amani. 

Bi. Mohammed aliwasikiliza wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na kuhimiza kwamba msaada uje haraka, hasa kwa wanawake na watoto walioathirika. 

Tweet URL

 

Migongano 

Aidha Bi. Mohammed amesisitiza wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Mataifa wa kukomesha mapigano na kuunga mkono mazungumzo ya kitaifa. 

Katika ziara hiyo ya mshikamano kwa Waethiopia, Amina Mohammed amesema ana uhakika wa kuwasili kwa amani. 

Alipoulizwa kuhusu jukumu la upatanishi la Muungano wa Afrika, Bi. Mohammed ameeleza kuwa viongozi wa kikanda na wengine wamelizungumzia  suala hilo. 

Mazungumzo 

Amina Mohammed alikuwa Afar baada ya kutembelea Tigray akiwa na Mjumbe Maalum wa Muungano wa Afrika, Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.   

Huku mazungumzo yakiendelea, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anabainisha kuwa kuna mapigano machache kuliko miezi michache iliyopita. 

Kwa upande wake anaona hali sasa ni "bora zaidi na kuna mazungumzo mengi zaidi" kuhusu mjadala wa kitaifa na njia ya amani nchini Ethiopia. 

Pia amesisitiza kwamba Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray kinashikilia madai ya usaidizi wa kibinadamu, kukomesha mapigano na kwa ajili ya mazungumzo.