Niger yahitaji msaada wa kimataifa; wakimbizi ni wengi: UNHCR na IOM
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM wametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Niger ambayo kwa sasa inahifadhi wakimbizi 250,000 kutoka nchi jirani huku ikiwa pia na wakimbizi wa ndani zaidi 250,000.