UNHCR yaonya ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wakimbizi
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kuhusu ongezeko la machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wakimbizi na wahamiaji katika mipaka mbalimbali ya nchi za Ulaya huku asilimia kubwa ya ukiukwaji huo ukisababisha vifo.