Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wanawake wakiwa wamejipanga mstari ili kupata chanjo dhidi ya Covid-19 nchini Malawi.
© UNICEF/ Thoko Chikondi

Omicron ilichochea wimbi la Covid-19 barani Afrika lakini inapungua haraka 

Baada ya wimbi la ugonjwa wa Covid-19 lililodumu kwa takribani wiki sita, wimbi hilo la nne barani Afrika ambalo kimsingi lilichochewa na mnyumbuliko wa virusi vya corona kwa jina Omicron, sasa linapungua na hivyo kulifanya kuwa wimbi lililodumu kwa muda mfupi zaidi katika bara hilo ambako jumla ya maambukizi hivi sasa tangu kuibuka kwa ugonjwa huo limezidi milioni 10. Imeeleza taarifa ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika iliyotolewa hii leo Brazzaville nchini Congo.  

Sauti
2'23"
Utepe mwekundu- ishara ya kimataifa ya kampeni ya kupambana na VVU na UKIMWI
Public Health Alliance/Ukraine

Ninaishi na VVU lakini nina afya njema na uwezo mkubwa wa kazi. Msitubague - Wu Megnam

Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO limeendelea mara zote kuhamasisha mazingira mazuri ya kazi ikiwemo kutokuwepo kwa ubaguzi au unyanyapaa kwa wafanyakazi kutokana na hali zao iwe ulemavu au ugonjwa.  Kisa hiki cha  Wu Mengnan wa China, ambaye miaka 15 iliyopita yeye na mumewe walipimwa na kukutwa na Virusi Vya UKIMWI, VVU kinaonesha kuwa bado kuna haja ya kufanya zaidi ili kukomesha ubaguzi na unyanyapaa mahali pa kazi au wakati wa kutafuta ajira. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.

Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.
UN Somalia

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia, Umoja wa Mataifa walaani

Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya UN amesema Shirika hilo linalaani shambulizi la kujitoa muhanga lilitokea leo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, akiongeza kusema, tunatoa "rambirambi zetu kwa familia za waathiriwa," na akawatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa. 

Muuguzi akimfanyia uchunguzi mjamzito wakati wa kliniki katika kituo cha afya nchini Uganda.
© UNICEF/Zahara Abdul

Asante UNICEF na wadau wa afya, ningekufa wakati wa kujifungua – Alice Aromorach 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la AVSI kutokana na ufadhili wa shirika la misaada ya maendeleo ya kimataifa la Sweden, SIDA, wamewezesha uwepo wa vyumba 10 kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa uangalizi mkubwa zaidi katika vituo vya afya katika mkoa wa West Nile nchini Uganda ili kutatua matatizo ya huduma za afya yaliyokuwa yanachangia uwepo wa idadi kubwa ya vifo vya wajawazito. John Kibego aliyeko Uganda anaeleza zaidi. 

Sauti
2'9"