Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi ya Friends of Mothers yadhamiria kuwainua wanawake nchini Uganda

Kahawa
Kahawa
Kahawa

Taasisi ya Friends of Mothers yadhamiria kuwainua wanawake nchini Uganda

Wanawake

Taasisi ijulikanayo kwa jina na Marafiki wa akina mama au Friends of Mothers iliyoko Mbale nchini Uganda imefanikiwa kuinua maisha ya zaidi ya familia 200 kutoka vijiji 7 baada ya kuwapatia ajira kwenye sekta ya kilimo. 

Muasisi wa asasi hiyo ni Massa Charles Frank ambaye anasema angali akiwa kijana mdogo alikuwa na ndoto ya kuwainua wanawake na ndio iliyompa hari ya kuianzisha. Akiwa ni mzaliwa wa eneo lenye mandhari nzuri ya milima na ukijani uliopambwa na zao la kahawa taasisi yake imejielekeza katika biashara ya zao  hilo. 

“Anasema , kuwainua wanawake ndio msingi mkuu wa biashara yetu, na tunafanya hivi sababu kuna umbwe la kijinsia, hakuna usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika biashara.” 

Jumla ya wanawake 200 kutoka katika vijiji 7wanafanya kazi na taasisi hii lakini si wao pekee bali wao na waume zao.“Wanawake wengi hawana mashamba lakini ni wakulima wetu na hii ni sababu wanandoa wamekubali kuwa mwanamke ndio awe mstari wa mbele. Wana umakini zaidi kwenye vitu vidogo, kitu ambacho wanaume hawana na hii inathibitika kwenye ubora wa kahawa tunayo izalisha.”

Mipango yao ya baadae ni kuwekeza katika kupata kiwanda cha kisasa zaidi. “ Tunataka kuendelea kuboresha biashara yetu kwa wateja wetu wa sasa lakini pia tunataka kuwavutia wateja wapya”.

Frank baada ya kuhudhuria mafunzo ya miezi 6 ya uwekezaji chini ya  Programu ya MARKUP yaliyoandaliwa na Muungano wa Ulaya na Afrika Mashariki na kisha kupatiwa mtaalamu wa kumuongoza kwenye uwekezaji, taasisi yake ilifanikiwa kupata mkopo wa dola 104,000 na sasa wamepanua uwanda wa miashara yao na bidhaa zao zinasafirishwa kwenda Canada, Ulaya na Marekani.