Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia, Umoja wa Mataifa walaani

Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.
UN Somalia
Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia, Umoja wa Mataifa walaani

Amani na Usalama

Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya UN amesema Shirika hilo linalaani shambulizi la kujitoa muhanga lilitokea leo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, akiongeza kusema, tunatoa "rambirambi zetu kwa familia za waathiriwa," na akawatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa. 

Kuhusu taarifa zilizokuwepo awali kuwa katika walioathirika wamo pia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Dujarric amekanusha akisema, "kinyume na ripoti za awali za vyombo vya habari, nadhani zilisema kwamba kulikuwa na baadhi ya maafisa wa Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa au wakandarasi katika msafara. Hawakuwapo.” 

Baadhi ya vyombo vya habari vinasema takriban watu wanane wamepoteza maisha katika mlipuko huo wa bomu ambao umetokea katika barabara iliyo karibu na kambi ya jeshi la wana anga wa Somalia na ambako pia ni karibu na uwanjawa wa ndege wa kimataifa, Mogadishu.