Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuondoa mabomu ya ardhini Sudan Kusini eneo sawa na viwanja 64 vya soka limesafishwa - UNMISS

Mfanyakazi wa UNMAS akondoa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Sudan Kusini. (Maktaba)
UN Photo / Isaac Billy
Mfanyakazi wa UNMAS akondoa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Sudan Kusini. (Maktaba)

Kuondoa mabomu ya ardhini Sudan Kusini eneo sawa na viwanja 64 vya soka limesafishwa - UNMISS

Amani na Usalama

Nchini Sudan Kusini kwa mwaka jana pekee wateguaji wa mabomu ya ardhini wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusafisha eneo lenye ukubwa sawa na viwanja 64 vya mpira wa miguu, na hivyo kuondoa hatari nyingi za milipuko, inaeleza UNMISS ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.

Kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini (UNMAS) asilimia 70 ya vilipuzi ambavyo vilikuwa havijalipuka sasa vimeharibiwa au kuondolewa katika maeneo vilimokuwa na hivyo kuwahakikishia watu makazi salama na maeneo ya kilimo. .

Mike Fula Rashid, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Sudan ya Hatua dhidi ya Vilipuzi (NMAA) anapeleka shukrani kwa Umoja wa Mataifa akisema,

"Tunashukuru kwa msaada ambao UNMAS inatupatia kuhusiana na uondoaji wa vilipuzi kwa sababu ukiangalia uwezo wa kuondoa mabomu nchini Sudan Kusini, asilimia 70 inaungwa mkono na UNMAS huku wafadhili wengine wakichangia asilimia 30 iliyobaki."